Subscribe:

Ads 468x60px

Labels

Bond: Jamani Nibembelezeeni Wastara Nimuoe!

KUTOKANA na ugumu wa masharti aliyopewa na mwigizaji Wastara Juma juu ya kumuoa, msanii Bond Suleiman ‘Bond’ ameomba msaada kwa watu wa karibu hususan upande wa Wastara kumsaidia kumuweka sawa ili atimize lengo lake la kumuoa.

Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Bond alisema Wastara ni mwanamke mwenye kila sifa ya kuwa mke, hivyo endapo atamkosa litakuwa ni pigo kubwa maishani mwake.

Jamani, amenipa masharti magumu sana, ni mwanamke thabiti ambaye nisingependa kumkosa, najaribu kuwatumia watu wetu wa karibu kumuweka sawa, maana ana kila sifa za kuitwa mke, nimekaa naye muda mrefu kama meneja wake, nimegundua mambo mengi sana, nahitaji msaada jamani,” alisema Bond.

Chanzo: GPL

0 comments:

Post a Comment

Asante kwa kusoma habari hii! Tafadhali acha tupia maoni yako HAPA!