Subscribe:

Ads 468x60px

Labels


Featured Posts

Shambulio la Dar es Salaam:Maswali muhimu ambayo hayajajibiwa kuhusu shambulio la bunduki

t

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Siku ya jana, jiji la Dar es Salaama, Tanzania lilisimama kwa muda kufuatia mtu mmoja kufanya mashambulizi ya risasi na kusababisha vifo vya watu wanne; askari polisi watatu na mlinzi mmoja wa kampuni binafsi ya ulinzi ya SGA.

Baadaye mtu huyo aliuawa na Polisi, mbele ya geti la ubalozi wa Ufaransa nchini humo, katika barabara ya Al Hassan Mwinyi, baada ya majibizano ya risasi yaliyodumu kwa dakika kadhaa.

Kwa Mujibu wa Mkuu wa operesheni za polisi, Liberatus Sabas, akitoa taarifa za awali alisema mbali na vifo hivyo pia watu sita walijeruhiwa.

Tangu kutokea kwa tukio hilo, kumekuwa na taarifa nyingi zikisambaa mtandaoni kuhusu tukio hili na maswali mengi yakiibuka, lakini kati ya hayo maswali haya manne yanaendelea kusubiri majibu

1: Mshambuliaji huyu ni nani?

Licha ya kusambaa kwa jina na picha za mtu anayedaiwa kuhusika na tukio hilo, Jeshi la polisi halijajitokeza mpaka sasa kumtaja ni nani hasa.

  • Je ni raia wa Tanzania ama kutoka nje ya Tanzania? anajishughulisha na nini hasa?

Duru pia zinaonesha kuwa askari polisi jjijini Dar es Salaam wameichukua familia ya mtu ambaye amekuwa akidaiwa kutekeleza shambulio hilo. Hata hivyo polisi nchini humo haijathibitisha iwapo familia hiyo imechukuliwa kwa ajili ya mahojiano ama kulinda usalama wao kutokana na kusambaa kwa picha za mtu huyo mitandaoni.

Hakuna mwenye uhakika wa asilimia 100 juu ya mshukiwa huyo, ingawa mashuhuda na wengine wanaojitokeza wanajaribu kuelezea haiba yake.

"Nilivyoenda baharini, tukakutana na yule mtu kavaa shati ya drafti ya mikono mifupi', anasema mama mmoja mbele ya vyombo vya habari vya Tanzania aliyedai kukutana na mtu huyo dakika chache kabla ya kuanza kushambulia."

"Tulivyokutana naye, yule mtoto mdogo kamsalimia, yule baba kapokea, ila Kiswahili chake sio cha huku (Tanzania)," aliongeza shuhuda huyo.

Mshambuliaji huyu anaongea Kiswahili ila kwa mujibu wa mama huyu Kiswahili chake hakijanyooka akimaanisha kama sio cha Tanzania. Swali hapa, Kiswahili chake sio cha Tanzania;

  • Je ni Kiswahili cha nchi gani?
  • Je inawezekana ametoka nchi nyingine zinazozungumza Kiswahili?
  • Je hakuna watanzania wenye kuzungumza Kiswahili kwa lafudhi isiyo ya lahaja ya kawaida?

2: Alipata wapi silaha?

Swali lingine linaloibuka hapa ni wapi mtu huyu alipata silaha za kufanya mashambulizi haya?

Taarifa za awali za polisi zinasema alipora bunduki mbili za askari aliowaua kwa bastola, lakini je bastola inayodaiwa kutumika kuwaua askari hao aliipata wapi?

  • Anaimiliki kihalali?
  • Ni mtu mwenye uwezo kifedha na mali kiasi cha kuhitaji kumiliki silaha?
  • Au ana maadui wengi?

Kumiliki silaha Tanzania inaruhusiwa kwa kufuata utaratibu, lakini wanaomiliki silaha wengi nchini humo ni watu wenye nafasi za juu kiungozi ama kimaisha.

  • Je mtu huyu alikuwa na sifa hizo?

Hakuna mwenye uhakika, Jeshi la Polisi litasema.

3: Alikuwa na dhamira gani hasa?

Hili ni swali muhimu ambalo majibu yake yanaweza kutoa picha ya hasa kwa nini mshambuliaji huyu aliamua kufanya mashambulizi yale na kusababisha vifo vya Polisi watatu na mlinzi mmoja, kabla na yeye kuuawa.

Inawezekana angekuwepo hai, angekuwa na majibu ya uhakika wa dhamira ya kufanya alichokifanya, lakini swali la alikuwa na dhamira gani? Mpaka sasa linasalia vichwani mwa watu.

Wakati umma wa watanzania ukisubiri taarifa rasmi za Jeshi la Polisi, labda kwa uchunguzi wao wanaweza kusema dhamira ni nini hasa, wapo wanaolitazama tukio hilo na kulihusisha na ugaidi na wengine kuhusisha na visasi. Hakuna ushahidi na uthibitisho wa hilo.

Lakini wapo wanaohoji kama tukio la kigaidi;

  • Kwa nini mtu huyu hakuonekana kuwalenga raia?
  • Licha ya kwamba alikuwa na nafasi, silaha na muda wa kutosha wa kufanya hivyo?
  • Kwanini hakuwashambulia raia?
  • Na kama ni kisasi, kwanini askari?
  • Ambao ni walinzi wa watu na mali kisheria?
  • Au aliwaona ni watu ambao wangeweza kumdhuru?

"Ni mapema sana kusema ni kwanini mtu huyu ameenda kufanya vile, uchunguzi utabaini," alisema Mkuu wa operesheni za polisi, Liberatus Sabas na kuthibitisha kwamba wameshaanza uchunguzi.

4: Kwanini mashambulizi katika eneo hilo?

Kwa mujibu wa taarifa za Polisi tukio hili limetokea katika makutano ya barabara ya Kenyatta na Kinondoni, alipoanza kuwashambulia askari na kuchukua bunduki zao zinazoonekana ni aina ya AK47, kabla ya kuelekea mbele ya ubalozi wa Ufaransa na kutumia kibanda cha nje ye geti la ubalozi huo kujificha akiendelea kushambuliana na Polisi. Amefia hatua chache kutoka kwenye geti la ubalozi huo.

Lakini eneo lilipotokea tukio hili, kwa mfano alipoanzia kuwafyatulia risasi Polisi na kuwaua ni pembeni ya makazi ya balozi wa Uingereza nchini Tanzania na pembeni ya barabara hiyo kuna ubalozi wa Urusi.

Eneo alipofia mshambuliaji huyo ni kwenye geti la ubalozi wa Ufaransa, eneo ambalo si mbali na makazi ya balozi wa Zambia, ubalozi wa Kenya na makao makuu ya benki ya KCB na Benki ya Stanbic.

Lakini pia si mbali sana na kilipo kituo cha Polisi cha Salender. Unaweza kujiuliza uthubutu gani alioupata mshambuliaji huyu, kiasi cha kwenda kufanya mashambulio hayo kwenye eneo la aina hii, ambalo kawaida ulinzi wake mkubwa haufanani na maeneo mengine?

  • Kuna mtu yuko nyumba yake?

Mbali na kusema ni mapema kusema dhamira ya mtu huyo kufanya mashambuli hayo nini, Mkuu wa operesheni za polisi, Liberatus Sabas alisema 'uchunguzi utabaini', na kuthibitisha kwamba Jeshi la Polisi limeshaanza kufanya uchunguzi wake.

Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 27.08.2021: Ronaldo, Mbappe, Kane, Kounde, Traore, Aubameyang

Cristiano Ronaldo

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, 

Cristiano Ronaldo alijiunga na Juventuskwa mkataba wa thamani ya euro milioni 112 (£99.2m) mwaka 2018

Manchester City na Juventus zimekubaliana kuhusu uhamisho wa mshambuliaji mreno Cristiano Ronaldo, 36, kujiunga na klabu hiyo ya City. (AS - in Spanish)

Juventus wanataka kati ya £21m-25m kwa ajili ya Ronaldo, huku City ikitarajiwa kumpa mkataba wa miaka 2. (Guardian)

Klabu hiyo ya Italia inatarajia Ronaldo atabakia klabuni hapo lakini wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa City mbrazil Gabriel Jesus, 24, kama mbadala wake. (Sky Sports)

Wolverhampton Wanderers imekataa ofa ya mkopo kwa ajili ya winga wake raia wa Hispania Adama Traore, 25, kutoka Tottenham Hotspur, wakitaka kumbakiza. (Telegraph)

Maelezo ya picha, 

Winga wa Wolverhampton Wanderers Adama Traore

West Ham United inamnyemelea mshambuliaji wa CSKA Moscow na Croatia Nikola Vlasic, 23, wakiendelea kutafuta mbadala wa kiungo mshambuliaji wa Manchester United na England Jesse Lingard. (Sky Sports)

Watford imeanza mazungumzo na Tottenham kuhusu uwezekano wa kumsajili kiungo mfaransa Moussa Sissoko, 32. (Fabrizio Romano)

Paris St-Germain inaendelea kusaka wachezaji akiwemo kiungo wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 28, na mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 21, wakati huu wakijiandaa kumkosa Kylian Mbappe. (L'Equipe, via Mail)

Manchester United midfielder Paul Pogba

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, 

Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba

Real Madrid imeongeza dau lake kufikia £145m kwa ajili ya mshambuliaji wa Ufaransa na PSG Mbappe, 22, baada ya dau lake la awali la £137m kukataliwa. (Sky Sports)

Manchester United imemkosa winga wa timu ya taifa ya England chini ya miaka 21 Noni Madueke, 19, baada ya nyota huyo kusaini mkataba mpya na klabu yake ya PSV Eindhoven. (Mirror)

Nahodha wa Tottenham na England Harry Kane yuko kwenye mazungumzo kuhusu kuboresha mkataba wake. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28, anatarajia mshahara utakaofikia £400,000 kwa wiki kupitia maboresho hayo ya mkataba baada ya kuamua kusalia klabuni hapo msimu huu. (Times - subscription required)

Harry Kane

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, 

Harry Kane yuko kwenye mazungumzo kuhusu kuboresha mkataba wake

Chelsea wanakaribia kabisa kumsajili mlinzi wa Sevilla na Ufaransa Jules Kounde, 22, katika uhamisho utakaogharimu £42m. (Sky Italia, via Star)

Wakati huo huo mlinzi wa kati wa Chelsea Kurt Zouma, 26, atafanyiwa vipimo vya afya kabla ya mfaransa huyo kusaini mkataba wa miaka 5 West ham kwa uhamisho utakaogharimu £26m. (Sun)

Tottenham imeanza mazungumzo kwa ajili ya kumsajili kiungo wa Juventus na Marekani Weston McKennie, 22 uhamisho utakaogharimu £40mil(Independent)

Pierre-Emerick Aubameyang

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, 

Mikel Arteta ametupilia mbali uwezekano wa mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang kuondoka

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta ametupilia mbali uwezekano wa nahodha na mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang kuondoka klabuni hapo. (ESPN)

Everton inamtaka mshambuliaji wa Brighton mfaransa Neal Maupay, 25. (Sky Sports)

Manchester United inataka kusajili kiungo kabla ya dirisha la usajili kufungwa, lakini itawapasa kusubiri kuona kama wanaweza kumpata kiungo wa England na West Ham Declan Rice, 22. (Independent)

Vita vya Afghanistan: Mkataba wa amani ulioondoa majeshi ya Marekani


Baada ya kuondolewa kwa vikosi vya kimataifa, Taliban ilienea Afghanistan, ikidhibiti karibu kila mji na jiji. Kwa nini Marekani ilikubali kuondoka baada ya miaka 20 ya mapigano?

Mnamo mwaka 2001, Nato iliifurusha Taliban kutoka Kabul baada ya mashambulio ya 9/11 huko New York na Washington.

Hata hivyo karibu miongo miwili baadaye, viongozi wa kundi la wanamgambo wa Kiislamu wamerudi katika mji mkuu wa Afghanistan, wakipiga picha za kujifurahisha katika ikulu ya rais na karibu nchi nzima ikiwa chini ya udhibiti wao.

Pengine kinachoshangaza zaidi ni kwamba haikuwa ushindi wa kijeshi wa Marekani na washirika wake wa Nato ambao ulisababisha mabadiliko haya, bali makubaliano ya amani yaliyojadiliwa kwa uangalifu.

Ni nini kilisababisha makubaliano hayo, yaliyosainiwa chini ya rais mmoja na kutekelezwa na mrithi wake, kwenda vibaya sana? 

Kwanini Marekani iliweka makubaliano na Taliban?



Siku moja baada ya Minara Pacha kuanguka, wakati huo rais wa Marekani George W Bush aliahidi "vita hii itachukua muda na kutatua, lakini hatukosei kuhusu hilo, tutashinda". Kwa kweli, Marekani haikukaribia kupata ushindi wa kijeshi dhidi ya Taliban.

Ingawa kundi hilo, ambalo lilikuwa na wapiganaji wa al-Qaeda waliohusika na mashambulio ya 9/11, lilisukumwa nje haraka ya miji na Nato, ilitumia miaka kadhaa kujipanga tena na mnamo mwaka 2004 walikuwa katika nafasi ya kuanzisha uasi dhidi ya vikosi vya magharibi na serikali mpya ya Afghanistan.

Kwa kujibu kuongezeka kwa mashambulio, rais mpya wa Marekani, Barack Obama, aliongeza idadi kubwa ya wanajeshi mwaka 2009 na kufanya ongezeko la wanajeshi wa Nato nchini humo kufikia 140,000.


Hii ilisaidia kuwarudisha nyuma Taliban mara nyingine tena, lakini kwa athari ndogo ya muda mrefu.

Mgogoro ulipokuwa vita virefu kabisa vya Marekani, na kugharimu nchi kiasi cha dola bilioni 978 na gharama ya maisha ya watu 2,300, ilizidi kutopendwa na Wamarekani na wito wa kukoma kuhusika na vita hivyo ulikuwa mkubwa.

Wakati idadi ya wanajeshi wa Marekani waliouawa kwa mwaka ilikuwa ndogo baada ya kuhamia rasmi katika jukumu la mafunzo na msaada mnamo 2014, Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani alisema mnamo 2019 kwamba "zaidi ya wafanyakazi wa usalama wa Afghanistan 45,000 wamejitoa sadaka kuu" katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Kukabiliwa na hali hii, mrithi wa Obama, Donald Trump, alianza kuzidisha mazungumzo na Taliban, akitia saini makubaliano mnamo Februari 2020.

Lilikuwa ni jambo ambalo alikuwa na furaha kuzungumza kuelekea uchaguzi wa urais wa mwaka huo.

"Kwa kweli, tumetoka Afghanistan, kama unavyojua,"aliiambia Axios news. "Tumekuwa huko kwa miaka 19. Tutatoka."

Makubaliano yalisema nini?



Marekani ilikubali kuondoa wanajeshi wake waliobaki kutoka Afghanistan na Taliban ilisema haitakubali al-Qaeda au kikundi kingine chochote chenye msimamo mkali kufanya operesheni zao katika maeneo wanayodhibiti.

Pia ilisema kwamba wafungwa 5,000 wa Taliban watabadilishwa kwa wafungwa 1,000 wa kikosi cha usalama cha Afghanistan na vikwazo vitaondolewa dhidi ya kundi la wapiganaji wa Kiisilamu.

Makubaliano hayo yalishirikisha tu Marekani na Taliban, na mpango huo ulikuwa kwamba Taliban itajadili na serikali ya Afghanistan baadaye ili kujua ni vipi na nani ataiongoza nchi hiyo baadaye.

Vikosi vya usalama vya Afghanistan - vilivyofundishwa kwa gharama ya dola za Marekani bilioni 88.32 na zaidi ya wanajeshi 300,000 kwa nadharia, walikuwepo kudumisha hali hiyo wakati mazungumzo yakifanyika.

Rais Trump - ambaye aliuelezea kama "mpango mzuri" kulingana na mshauri wake wa Usalama wa Kitaifa wa wakati huo John Bolton - alisema hadharani kwamba mpango huo ulikuwa na "nafasi ya kuwa mzuri sana".

Pande zote mbili zilizingatia makubaliano ?



Marekani kwanza ilianza kuondoa wanajeshi chini ya Trump. Mazungumzo ya ana kwa ana kati ya Taliban na serikali ya Afghanistan yalianza mnamo Septemba, lakini suluhu haikuonekana kuwa karibu.

Licha ya ukosefu wa maendeleo, wapinzani wa Taliban walibaki wakishikilia kuwa mpango huo hautasababisha maafa.

"Hii sio Vietnam," rais wa Afghanistan aliiambia BBC mnamo Februari. "Hii sio serikali inayoanguka."

Mnamo mwezi Julai, msemaji wa Taliban alidai "ingawa tuna nguvu juu ya uwanja wa vita, tunazingatia mazungumzo ".

Labda inaelezea zaidi kwamba walikuwa wakichukua miji mikuu 10 kwa wiki wakati huo.

Rais wa sasa wa Marekani Joe Biden - ambaye licha ya kutokubaliana na Trump karibu katika kila sera - aliendelea kutekeleza makubaliano ya mtangulizi wake, akiwaambia waandishi wa habari mwezi uliopita "hatapeleka kizazi kingine cha Wamarekani kupigana huko Afghanistan bila matarajio mazuri ya kufikia matokeo tofauti ".

"Uwezekano kutakuwa na Wataliban wanaotawala kila kitu na kumiliki nchi nzima kuna uwezekano mkubwa," ameongeza.

Na licha ya matukio ya siku za hivi karibuni, inaonekana rais amekwama na uamuzi wake.

"Ikiwa kuna chochote, maendeleo ya wiki iliyopita yanasisitiza kwamba kumaliza ushiriki wa jeshi la Marekani nchini Afghanistan sasa ilikuwa uamuzi sahihi," alisema Jumatatu.

Lakini kwa wengi, maoni ya kiongozi wa Taliban Mohammad Abbas Stanikzai akiongea katika chumba cha hoteli ya kifahari baada ya kusaini makubaliano na jeshi lenye nguvu zaidi ulimwenguni mnamo Septemba mwaka jana itakuwa ya kweli zaidi.

"Hakuna shaka tumeshinda vita," alisema. "Hamna shaka."

Credit: BBC

BASATA Watoa Maelezo ya Kwanini Limemfungia Shilole Kutojihusisha na Sanaa

Baraza la Sanaa la taifa, BASATA, limemfungia Shilole kutojihusisha na masuala ya muziki ndani na nje ya Tanzania kwa mwaka mmoja.
BASATA limempa barua Shilole jana yenye taarifa za kufungiwa kwake.
Adhabu hiyo imetolewa kufuatia tukio la msanii huyo kupigwa picha za aibu wakati akitumbuiza nchini Ubelgiji miezi kadhaa iliyopita.
Hii ni taarifa rasmi ya BASATA:
 Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kama msimamizi na mratibu wa sekta ya Sanaa nchini limemfungia msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Zuena Mohamed kwa jina la kisanii Shilole kufanya shughuli za sanaa nchini kwa muda wa mwaka mmoja kuanzia tarehe 24/07/2015 hadi tarehe 24/07/2016.
      Itakumbukwa kuwa mnamo tarehe 09/05/2015 akiwa katika onyesho lake la Muziki nchini Ubelgiji alikiuka maadili ya kazi ya sanaa mbele ya hadhira ya wapenda sanaa za Tanzania na hivyo akadhalilisha utu wake na jamii ya Kitanzania kimaadili.
Pia itakumbukwa kwamba mnamo mwezi Oktoba, 2013 BASATA ilimuonya na akakiri kwa kuomba msamaha kwa tabia yake ya kucheza bila kuzingatia utu na maadili awapo jukwaani.
BASATA ilimpa nafasi ya kutoa maelezo yake kwa nini asichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kitendo chake cha kudhalilisha maadili, utu na sanaa ya Tanzania lakini akakaidi kutoa maelezo. Hivyo basi BASATA imejiridhisha kwamba alikiuka maadili ya kazi ya sanaa kwenye onesho lake la huko Ubelgiji makusudi na amekiuka Sheria, Kanuni na Taratibu za uendeshaji wa Sanaa.
Hivyo basi kutokana na ukiukwaji huo wa sheria na kanuni za uendeshaji wa shughuli za sanaa nchini, Baraza la Sanaa la Taifa chini ya Kanuni ya 30(1)(d) ya G.N 322 ya 2005 limemsimamisha kujishughulisha na kazi za Sanaa nchini kwa muda wa Mwaka Mmoja tokea tarehe 24/07/2015.
Hivyo haruhusiwi kufanya au kushiriki kwa namna yoyote ile shughuli yoyote ya onesho la sanaa nchini au nje ya nchi. Iwapo atafanya kinyume cha hayo kutapelekea kupewa adhabu zaidi ikiwa ni pamoja na yeyote yule utakaye shirikiana naye.
Ni matumaini ya Baraza la Sanaa la Taifa kwamba wasanii na waandaaji wa shughuli za sanaa wataendelea kutambua umuhimu wa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa.
      Shilole aliwahi kusema kuwa hata yeye hakupenda kile kilichotokea jukwaani wakati akitumbuiza nchini humo kwa sababu ilikuwa bahati mbaya na hakudhamiria kukaa uchi kama wengi wanavyosema.
Shishi ambaye ni mama wa watoto wawili alisema kuwa nguo mpya aliyoivaa siku hiyo ndio ilimponza kwasababu hakuwa ameifanyia majaribio ya kutumbuiza akiwa ameivaa.
“Kiukweli kwasababu hili jambo limetokea inatakiwa nguo ninapoinunua niwe naifanyia training kwanza kabla ya kwenda jukwaani, kwahiyo kwasababu ile nguo ilikuwa mpya kwangu na sikuweza kuijua vizuri […] yaani hii nguo nimeikuta huku huku, nguo imekuja kunitokea bahati mbaya wakati niko kwenye performance, ilitatuka wakati niko kwenye motion,” Shishi aliiambia Clouds FM.
Aliongeza kuwa alisikitishwa na mtu aliyempiga picha hizo na kuamua kuzisambaza mtandaoni bila kujua kuwa itamuumiza yeye kama mwanamke.
“Nasisitiza tena sikudhamiria na wala sikupenda hiyo kitu itokee, ila nasikitika kwamba kama mimi mwanamke yule mtu aliyenipiga picha na kudhamiria kuziweka kwenye mitandao alikuwa na maana gani, hakufikiria mimi nitaunmia kiasi gani au mashabiki wangu wataumia kiasi gani? Ni mtu mbaya mwenye roho mbaya sijui nimuiteje huyo mtu aliyefanya hivyo, sio mtu mzuri.”
Unachukuliaje adhabu hiyo? Ni halali ama Shilole ameonewa?
                                                                                                         Chanzo:Bongo5

Kuna wakati natamani sana... - DAVINA

“MOYO wangu umegandwa na mavumbi, macho yamepofuka kwa machozi, kwani mateso yangu hayapimiki kwa mizani, kila mtu ananihukumu kwa uongo na hadithi za kutunga juu ya ndoa yangu pasipo kujua ukweli,” ndivyo anavyoanza kusimulia staa wa filamu za Kibongo, Halima Yahya ‘Davina’ akielezea wakati mgumu anaokutana nao baada ya kuwepo na mgogoro kwenye ndoa yake.
Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu hivi karibuni, msanii huyo alisema kila mahali anapopita ananyooshewa vidole kwa watu kumhukumu kuwa ni mkorofi kwenye ndoa yake jambo ambalo halina ukweli.
Akaeleza kuwa, siri za ndoa huzijua wahusika na kwamba hata yeye kufikia hatua ya kutengana na mumewe anajua chanzo ni nini na si rahisi kumueleza hata mama yake mzazi, ila watu wanatumia maneno makali yanayomuumiza.
“Kila mtu anasema analolijua, hakuna aliyenilazimisha kuolewa, kilichonifarakanisha na mume wangu tunakijua sisi wawili (yeye na mumewe), labda na watu wangu wa karibu, lakini kwa sasa maneno yamekuwa mengi sana, tena yenye kuumiza kiasi kwamba kuna wakati natamani hata kujitoa uhai.
“Vitu vingine ni vya ndani sana hata mama yangu mzazi siwezi kumwambia, ila maneno yamenizidia, haya, huyo Mike wanayemsema natoka naye, jamani nimemjua Mike kabla ya mume wangu, ilikuwaje nisitoke naye zamani ije kuwa leo? Naumia miye jamani, Mungu anajua, ipo siku kila kitu kitakuwa wazi,” alisema Davina kwa sauti ya uchungu.


Chanzo: Bongomovies

Wastara: Yusuph Mlela Anafanana Vitu Vingi na Sajuki

Staa wa Bongo Movies, Wastara Juma amefunguka na kumwagia sifa muigizaji mwenzake, Yusuph Mlela kuwa ni mtu ambaye anafanana vitu vingi na aliyekuwa mume wake, marehemu Sajuki  na kusisitiza kuwa huwa hachoki kufanya naye kazi.

Kupitia ukurasa wakekwenye mtandao wa instagram, Wastara aliweka picah hiyo hapo juu na kuandika;

Mama na mwana mama na baba nimeipenda kama ilivyo ila truelly huyu jamaa nampenda mfano hakuna mpole muelewa hana makuu anao ubinadaamu hana ugomvi na mtu mpole hajui kufoka wala kugombana akikasirika dakika 2 tu anarudi kuwa normal sichoki kufanya naye kazi namchukulia ni mdogo wangu wa tumbo moja namfananisha vitu vingi na Sajuki si mwingine this is Yusuph Mlela au Mlelandro

CHUCHU HANS NI WIFE MATERIAL - VINCENT KIGOSI (RAY)

Muigizaji mahiri wa kiume hapa Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’amefichua siri iliyomfanya kunasa kwa staa mwenzake Chuchu Hans, na hata kupata msukumo wa kumuweka hadharani tofauti na tabia yake ya nyuma ya kutopenda kumuanika mpenzi wake.
Akizungumza na gazeti la Risasi akiwa kwenye tamasha la kimataifa la Filamu ‘ZIFF’ lililofanyika visiwani Zanzibar, Ray alisema kilichomsukuma kumuanika Chuchu ni mambo yake adimu ambayo huwezi kupata kwa mwanamke mwingine.
     Alisema anamuona kuwa na tabia zote za mke, ndiyo maana aliweza kumtambulisha kwa jamii kwa kuwa ana imani naye kwa kila kitu hivyo yuko huru watu kumfahamu.
        “Bwana huyu mwanamke ana vitu vyake adimu sana, na kwa kweli nampenda na ana chembechembe zote za kuwa mke ndiyo maana nilikuwa huru kumuweka wazi bila wasiwasi wowote,” alisema Ray ambaye pia aliwahi kutoka kimapenzi na Johari.

Chanzo:GPL