WALE wasanii wawili waliodumu kwenye uchumba kwa
muda mrefu, Ramadhan Baba ‘H.Baba’ na Flora Mvungi wameamua kuvunja ukimya na
kutangaza rasmi kuwa wanatarajia kufunga ndoa Juni 8, mwaka huu.
Akizungumza
na Ijumaa hivi karibuni, Flora alisema wale waliokuwa wakidhani uchumba wao ni
geresha walie tu kwani siku ya kutimiza ndoto yao ya kuishi kama mke na mume
imekaribia.
“Tuko
kwenye maandalizi ya ndoa yetu baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, sasa
tumeamua kufunga ndoa na sherehe ya ndoa itafanyika Juni 8, sendoff Juni 4
mwaka huu ikiwa Mwenyezi Mungu atatujaalia uzima,”alisema Flora ambaye kwa sasa
ni mjamzito.
0 comments:
Post a Comment
Asante kwa kusoma habari hii! Tafadhali acha tupia maoni yako HAPA!