FREEMASONS ni jamii ya siri (secret society) inayotisha duniani,
njama zao za kuitawala dunia ifikapo Desemba 2012 ni tisa, kumi ni
unyama wa kutisha waliomfanyia aliyekuwa Kiongozi wa Libya, Muammar
Gaddafi.
Memba wa Freemasons hususan wale wanaomuabudu Shetani, Lucifer (Jini
Mkuu), wanadaiwa kumchana Gaddafi kifuani, wakaikinga damu yake na
kuihifadhi kwenye glasi kabla ya kuitumia katika kafara nzito.
Mtandao mmoja wa kidini umeandika kuwa damu ya Gaddafi, ilichanganywa
na ya mbuzi aliyechinjwa ili kutolewa kafara katika kuadhimisha
kukamatwa, kuteswa na hatimaye kuuawa kwa Gaddafi.
Katika habari
hiyo, ilielezwa kuwa Freemasons walichukua kiasi kidogo cha damu ya
Gaddafi na kuimimina kwenye ile ya mbuzi ambayo ndiyo ilikuwa nyingi na
kuhifadhiwa kwenye chombo kimoja.
Habari zinafafanua kwamba baadhi ya Freemasons walikunywa, wengine
walilamba na kunawa katika kusherehekea kuingiza mizizi yao ndani ya
nchi yenye utajiri mkubwa wa mafuta (Libya).
Hata hivyo, kati ya wafuasi waliohudhuria kafara hiyo ni idadi ndogo mno
waliokunywa damu ya Gaddafi iliyochanganywa na ya mbuzi, kwani wengi
walilamba na kunawa, ikiwa ni ishara ya kutambua utukufu wa kiongozi
wao, Lucifer.
“Damu iliwekwa kwenye glasi, aliyetaka kunywa, alimimina kidogo kwenye
glasi ya peke yake, waliolamba waliingiza vidole na kulamba kisha
wakanawa,” uliandika mtandao huo.
Kwa mujibu wa mitandao inayochambua mambo ya Freemasons, jamii hiyo ya
siri hupenda damu ndiyo maana maadhimisho yao husindikizwa na kafara ya
kuchinja wanyama hususan mbuzi.
Maalim Hassan Yahya Hussein ambaye ni mnajimu mwenye utaalamu mkubwa wa
falsafa za Freemasons, naye alilithibitishia gazeti hili kuwa jamii hiyo
hupenda damu kwa sababu humfurahisha kiongozi wao mkuu, Lucifer.
“Kuchinja na kuona damu kuna maana kubwa mno kwa Freemasons, wanapenda sana damu,” alisema Maalim Hassan.
NJAMA NI ILE ILE
Inaelezwa kuwa Freemasons ipo kwenye mkakati thabiti wa kuitawala dunia
kabla ya Desemba 2012, hivyo imekuwa ikiratibu sera zake kwa kuangusha
tawala za nchi mbalimbali ambazo viongozi wake wameshindwa kuendana na
matakwa yake kama ilivyokuwa kwa Gaddafi.
Maalim Hassan aliliambia Uwazi: “Freemasons inapambana kutwaa mamlaka ya
nchi tajiri kama Libya, inawaondosha viongozi ambao hawaendani na
matakwa yao. Shabaha ya Freemasons pia ni kupambana na Uislam pamoja na
Ukristo.
“Ipo wazi kuwa lengo lao ni kuitawala dunia, kwa hiyo wanasimamia kuona
hilo linawezekana kwa kuhakikisha Uislam na Ukristo unaishiwa nguvu na
Shetani anashinda hapa duniani,” alisema Maalim Hassan ambaye ni mrithi
wa kazi za marehemu Sheikh Yahya.
Aliongeza: “Mkakati mkubwa zaidi ni kuhakikisha dunia inaabudu Dini ya
Shetani, wanataka kila mtu awe chini ya mamlaka ya Jini Mkuu, Lucifer.
Dunia nzima itawaliwe na serikali moja na iwe na sarafu moja.”
AFRIKA MASHARIKI YACHIMBWA
Kuangushwa kwa Gaddafi siyo suala la mzaha kwa Afrika, kwani inadaiwa
kuwa Freemasons kupitia Jeshi la Kujihami la Nchi za Magharibi (Nato),
inatekeleza sera zake kwa vitendo kwa nchi ambazo viongozi wake
wameshindwa kukidhi matakwa yao.
Inaelezwa kuwa Freemasons hawapendi nchi kuungana na kubainisha kuwa
ndiyo maana wameanza kuichimba Jumuiya ya Afrika Mashariki na ili
kuidhoofisha, wameingiza agizo la kukubali ndoa za jinsi moja.
Habari zinasema kuwa Serikali ya Uingereza imekuwa ya kwanza kutumiwa na
Freemasons katika kuhakikisha nchi zote zinazounda Jumuiya ya Madola
zinapitisha sheria zinazokinzana na maandiko matakatifu yanayoaminiwa na
waumini wa Dini za Kiislam na Kikristo.
Imeelezwa kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki nguzo yake ni Tanzania, Kenya
na Uganda ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Madola, hivyo agizo la ndoa
za jinsi moja lengo lake ni kuzigawa kati ya zile zitakazokubali na
zitakazokataa ili mwisho wake ziwe na mfarakano.
Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (Saut),
Profesa Mwesiga Baregu, alizungumza kupitia runinga moja hivi karibuni
kuwa anguko la Gaddafi Libya ni ishara mbaya kwa vyama vikongwe kama
Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Alisema, nchi za magharibi hazipendi kuona vyama vikongwe vikishika
madaraka kwa muda mrefu, kama ilivyo kwa CCM ambacho kinaongoza nchi
tangu uhuru (Tanganyika mwaka 1961, Zanzibar 1964), kikiwa ni mtoto
aliyezaliwa baada ya Tanu na ASP kuungana.
Angalizo hilo la Baregu, linatishia pia amani ya utawala wa Rais wa
Uganda, Yoweri Museveni na chama chake cha National Resistance Movement
(NRM), kwani yupo madarakani kwa miaka 25 sasa (alianza kutawala Januari
26, 1986).
Rais wa Kenya, Mwai Kibaki na chama chake cha People National Unit (PNU)
ndiyo anapona kwenye angalizo hilo, kwani kuna mabadiliko makubwa ya
vyama tawala nchini kwake, katika mihula miwili kati ya mwaka 2002 na
2012, tayari vimeshaongoza viwili. (Mwaka 2002 hadi 2007, chama tawala
kilikuwa Narc).
VITA YA IMANI
Maandiko yanasema kuwa nyakati za mwisho kutakuwa na tishio la dunia
kutawaliwa na Dini ya Shetani ambapo zama hizo zikifika kutakuwa na
mfumo utakaozuia mtu yeyote kupata huduma za kijamii mpaka awe
mwanachama na atatambulika kwa chapa 666.
Habari zaidi zinaeleza kuwa Freemasons wanatumia njia mbalimbali
kuhakikisha ulimwengu mzima hakuna anayeamini dini za Mungu na
wanapambana kuhakikisha hata Yesu (Nabii Isa) atakaporejea akute hakuna
aliye tayari kukombolewa.
Katika kuhakikisha wanapambana na nguvu ya Yesu, Freemasons wamekuwa
wakitumia damu ndiyo maana hutoa kafara kwa kuchinja wanyama hasa mbuzi
au kondoo wenye pembe zinazotengeneza alama ya V kwa imani kwamba
huwaongezea nguvu ya kuishika dunia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Asante kwa kusoma habari hii! Tafadhali acha tupia maoni yako HAPA!