STAA wa filamu za
Kibongo, Lungi Mwaulanga hivi karibuni aliswekwa lupango katika Kituo cha
Polisi Oysterbay jijini Dar baada ya kuzushiwa kesi ya ujambazi na mpangaji
mwenzake .
Akizungumza na waandishi wetu,
Lungi aliyesota mahabusu kwa siku mbili alisema hivi karibuni usiku wa manane
aligongewa mlango nyumbani kwake na watu asiowafahamu, alipotoka alikutana na
askari waliomchukua na kumwambia kwamba anatuhumiwa kwa ujambazi.
Hata hivyo, Lungi alisema kuwa
baada ya kuwauliza askari ni wapi dada huyo amevunjiwa au kitu gani
alichoibiwa, askari walimbadilishia kesi na kumwambia kuwa amemtukana. Mpaka
sasa, Lungi yuko nje kwa dhamana.
0 comments:
Post a Comment
Asante kwa kusoma habari hii! Tafadhali acha tupia maoni yako HAPA!