CLOUDS FM iliripoti kuhusu kushamiri kwa
Biashara ya Ngono katika Maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam
na jinsi serikali inavyolishughulikia tatizo
hilo linalokua kwa kasi....
Wakihojiwa kwa nyakati tofauti,
baadhi ya wasichana wanaojishughukisha na biashara hiyo wameelezea changamoto
mbalimbali wanazokutana nazo katika kazi hiyo hususani nyakati za usiku.
Wakizungumzia adha wanazokutana nazo Wasichana hao
wamesema kuwa licha ya kukabiliwa hali ngumu ya maisha iliyopelekea kuingia katika
biashara hiyo, bado wamekuwa wakikutana na matukio mabaya ikiwemo kukamatwa na
kuingiliwa kinguvu na baadhi ya watu wanaojitambulisha kwao kuwa ni askari wa
Polisi jamii. Mbali na hilo Wasichana hao wamesema hali ngumu ya
Maisha imekuwa ikiwalazimu kufanya mapenzi kinyume na maumbile wanapokuwa
kwenye Hedhi, pasipo kujali hatari ya kukumbwa na maradhi yoyote.
Hivi karibuni Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni
lilitangaza mpango wa kuwaondoa wasichana wamaojishughulisha na Biashara ya
ngono mitaani na kuwashtaki kwa mujibu wa Sheria ya makosa ya uvunjifu amani na
ukiukwaji wa maadili.
Wakizungumza baadhi ya wadau kutoka mashirika na
Taasisi mbalimbali za kutetea haki za Binadamu nchini, ambapo kituo cha Sheria
na haki za Binadamu pamoja na taasisi ya kutetea haki za Binadamu ya Chuo Kikuu
cha Tumaini, kimesema kuwa kitendo cha kuwakamata wasichana hao hakiwezi kuwa
suluhisho la kutokomeza Biashara ya ngono nchini.
Eneo la MANZESE Uwanja wa Fisi ni miongoni mwa
Maeneo ambayo Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam limeliainisha kuwa
limekuwa likikithiri kwa Biashara hiyo
Credit: Cloudsfm
0 comments:
Post a Comment
Asante kwa kusoma habari hii! Tafadhali acha tupia maoni yako HAPA!