Ni muda mrefu imekuwa ikisemwa kuwa wasanii wanaoendesha maisha yao
kwa ‘kuuza nyago’ kwenye filamu za Kibongo ni watu wanaojiuza, kufanya
ufuska na kupiga picha za utupu, ambapo imeshawahi kutolea orodha ndefu
ya wasanii hao, huku wengine wakiondoka nchini na kwenda kufanya ufuska
huo nje ya Tanzania.
Madai ya kufanya ufuska yaliwahi kuthibitishwa na msanii wa filamu Bongo, Coletha Raymond ‘Koleta" aliyesema kuwa “Kiukweli sanaa inatufanya wasanii wa kike tuingie kwenye vitendo vya umalaya. Sanaa ya Bongo ni vigumu sana kutoka, hailipi kabisa... yaani inatakiwa mtu ufanye kazi nyingine tofauti ndiyo uweze kufanikiwa. Wasanii unaowaona wamefanikiwa si kwa filamu pekee, wana mambo mengine,” alisema na kuongeza:

“Kwa bahati mbaya kuna wanaotaka kutumia njia ya mkato, hao wanajikuta wameangukia kwenye umalaya. Kwa sababu wanafanya mambo yao na jamii inawaona, wasanii wote wa kike tunahesabiwa ni malaya tu.”
Miezi
ya karibuni habari za kuaminika zilitolewa tena kuwa wasanii wengine
wawili wa filamu, Kelvina John na Edna Gabriel, walikuwa wanafanya
ufuska nchini Kenya ikiwa ni pamoja na kujiuza na kupiga picha chafu.
Chanzo
kimoja makini cha habari ambacho kipo nchini humo kiliwahi kutonya
kuwa, wasanii hao walikuwa wanafanya uchafu huo wakiwa jijini Nairobi ambako walikwenda kwa shughuli ambayo hadi sasa haikufahamika.
“Kwa kweli hawa mademu wamepinda, yaani wamediriki kupiga picha chafu wakiwa katika hoteli moja hapa Nairobi
na walikuwa wakijichanganya katika klabu ambazo baadhi ya wanawake
hucheza uchi na kujiuza, mimi kwa kuwa nawajua nilipowaona nilishangaa sana,” kilidai chanzo hicho.
Kikaongeza kuwa, walivyoonekana wasanii hao ni kama walikwenda kwenye jiji hilo kwa lengo la kufanya ufuska wakijua huko hakuna atakayewajua.
Katika
kuweka mambo sawa, mpekuzi wetu alimtafuta mmoja wa wasanii hao,
Kelvina kuzungumzia skendo hiyo na alipopatikana alikuwa na haya ya
kusema:
“Sisi tulipiga picha zetu wenyewe kwa matakwa yetu sijui kwa nini mtu alizichukua na kuwaletea? Na hilo suala la kuingia kwenye klabu za wacheza uchi tuliingia tu kama moja ya kumbi za starehe lakini siyo kwamba tulienda kucheza au kujiuza kama mlivyoambiwa.”
0 comments:
Post a Comment
Asante kwa kusoma habari hii! Tafadhali acha tupia maoni yako HAPA!