Mwenyekiti wa Lindi Press Club Ahmeid Abdulaziz kushoto akibadilishana mawazo na Daudi Mwangosi (Iringa).enzi za uhai wake. Wote ni Waandishi wa Channel 10 |
KUNA jambo moja linawasumbua watu na wapenda haki, namna ambavyo marehemu ameuawa.
Kwa
ufupi ni kuwa ‘BOMU LA MACHOZI’ halijakusudiwa kuuwa na watengenezaji
wake, lakini linapotumika isivyo sahihi huuwa, hiyo hakuna shaka
Marehemu DAUD MWANGOSI ameuawa na askari polisi.
Taarifa za awali kutoka katika eneo la tukio huko Nyololo,
wilayani Mufindi zineonesha kwamba amepigwa bomu hilo akiwa amekamatwa
na FFU.
Alipigwa bomu hilo baada ya kupokea kipigo kikali kutoka kwa baadhi ya askari waliokuwa wakizuia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kisiendeshe harakati zake za kufungua tawi katika eneo hilo.
Mwangosi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa (IPC), mbali na kuuawa mbele ya wananchi wa eneo hilo, walikuwepo pia askari Polisi wengi wa Kutuliza Ghasia (FFU) na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa (IPC).

Mwili wa marehemu Mwangosi umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya wilaya ya Mufindi.
Taarifa kutoka kwa Katibu Msaidizi wa IPC, Francis Godwin zinaonesha kwamba taratibu za kuutoa mwili huo kutoka katika hospitali hiyo zitafanywa baada ya wahusika kuufanyia uchunguzi.
Hakuna uthibitisho kwamba IGP Said Mwema atakwenda Mafinga, lakini taarifa zisizo rasmi kutoka Mafinga, zimedai kwamba kesho Septemba tatu atatua Mafinga kushiriki katika uchunguzi huo.
Baada ya kufanyiwa uchunguzi, mwili wa mpambanaji Mwangosi utasafirishwa hadi mjini Iringa na taratibu zingine zikiwemo za mzishi zitatangazwa baada ya familia yake kujadiliana.
Kabla ya kushiriki tukio hilo lililositisha maisha yake hapa duniani, Mwangosi aliongoza Mkutano Mkuu wa IPC uliofanyika Septemba 1, katika ukumbi wa Maktaba mjini Iringa.

Mkutano huo ulihitimishwa kwa wanachama wa IPC kukutana na kula chakula
cha jioni katika moja ya sehemu za burudani mjini Iringa.
Septemba 2, Mwangosi alishiriki Press Conference iliyoitishwa na RPC wa Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda na baadaye ile iliyoitishwa na Katibu Mkuu wa Chadema Dk Wilboroad Slaa.
Wakati RPC alipiga marufuku kufanya mkutano wowote wa nje mpaka zoezi la sensa litakapokamilika, Chadema waliahidi kuendelea na ratibu ya kukijenga chama chao mkoani Iringa.
Mwangosi hakuwa ameambatana na msafara wa Dk Slaa wakati ukielekea Mafinga. Taarifa zinaonesha kwamba baada ya kumaliza kazi zake zingine za kiuandishi majira ya saa saba na nusu mchana alipanda basi la Abood lililokuwa likitokea Dar es Salaam hadi Nyololo ambako chadema walikuwa na ratiba ya kufungua tawi.
Wakati wakifungua tawi hilo, wananchi walianza kukusanya na ndipo, Polisi wakatoa tahadhari iliyowataka watawanyike kwasababu shughuli ya ufunguzi wa tawi hilo ilikuwa inafanywa nje tofauti na maelekezo ya jeshi hilo.
Katika kurukushani hiyo mwandishi mmoja Godfre Mushi inadaiwa alikamatwa na Polisi wakati akipiga picha, na Mwangosi alipotaka kujua sababu za askari hao kumkamata naye alishambuliwa kwa virungu kabla hajalipukiwa na bomu hilo.
Mmoja wa askari wa jeshi hilo aliuumbaia mtandao huu kwamba kinachomtambulisha Mwangosi, ni kichwa na sura yake kwa kuwa havikudhuliwa na mlipuko wa bomu hilo, lakini sehemu nyingine za mwili wake zimesambaratika vibaya.

Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kwa kupitia Rais
wake Kenneth Simbaya tayari umetuma wawakilishi mkoani Iringa kwa ajili
ya kulifanyia uchunguzi wa kina tukio hilo na utatoa msimamo wake
Jumatano.
Na Jukwaa la Wahariri Tanzania kwa kupitia Katibu wake, Neville Meena umahidi nao kutoa tamko baada ya kupata taarifa za kina kuhusiana na tukio hilo.
IPC kwa upande wake inaendelea kushiriki uratibu wa msiba na kwa kushirikiana na wanahabari wote wa mkoa wa Iringa inaendelea kupokea michango mbalimbali kutoka kwa wasamalia wema.
Waandishi wa habari, viongozi wa serikali na taasisi binafsi wameeendelea kutoa rambirambi zao kupitia uonngozi wa IPC.

0 comments:
Post a Comment
Asante kwa kusoma habari hii! Tafadhali acha tupia maoni yako HAPA!