WATU wawili wamefaki dunia na wengine 42 kujeruhiwa katika ajali ya basi iliyotokea mjini Kahama, mkoani Shinyanga. Basi
hilo lilipunduka baada ya kumgonga mwendesha pikipiki ya abiria
'bodaboda', wakati likitokea mjini hapa kwenda Dar es Salaam, katika
eneo la Nyasubu. Ajali hiyo imetokea jana alfajiri ikihusisha basi
lenye namba za usajili T 391 BWP, aina ya Scania linaloitwa “Leina
Tours”, linalofanya safari zake kati ya Kahama na Dar es Salaam. Mmoja
wa majeruhi Bw. Kayumba Yusufu (52), mkazi wa Dar es Salaam, alisema
basi hilo liliaguka mda mfupi baada ya kutoka Stendi Kuu ya Mabasi mjini
Kahama, eneo Nyasubi jirani na Benki za Azania na NBC. Taarifa
iliyotolewa na Mganga Mkuu wa Wilaya, Dkt. Andrew Emmanuel, alisema
abiria mmoja aliyemtaka kwa jina la Happy John, mweye umri kati ya miaka
37-40, mkazi wa Tarime, mkoani Mara, alifariki hapo hapo. Alisema
dereva wa pikipiki Willison Paschal (24), ambaye inadaiwa ndiye
aliyesababisha ajali hiyo, naye alifariki dunia baada ya kufikishwa
hospitali kwa matibabu. Dkt. Emmanuel alisema majeruhi
waliofikishwa hospitari walikuwa 42, kati yao 27 waliumia vibaya na
kulazwa wakiwemo wanaume 15, wanawake 12 ambapo 15 walipatiwa matibabu
na kuruhusiwa.
Mkuu wa Polisi wilayani hapa, Bw. George Simba, alisema basi hilo lilikuwa likiendeshwa na Bw. Amini Amri, mkazi wa Dar es Salaam ambaye baada ya ajari alikimbia kusikojulikana.
Chanzo: Patrick Mabula, Kahama
Mkuu wa Polisi wilayani hapa, Bw. George Simba, alisema basi hilo lilikuwa likiendeshwa na Bw. Amini Amri, mkazi wa Dar es Salaam ambaye baada ya ajari alikimbia kusikojulikana.
Chanzo: Patrick Mabula, Kahama
0 comments:
Post a Comment
Asante kwa kusoma habari hii! Tafadhali acha tupia maoni yako HAPA!