Picha siyo Halisi |
MWANAFUNZI wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Hogolo, (jina
tunalo), mwenye umri wa miaka 14, ameuawa kwa kunyongwa baada ya kubakwa
na mwili wake kufukiwa katika shimo nyuma ya nyumba yao karibu na choo. Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Zelothe Stephen,
alisema tukio hilo limetokea Agosti 11 mwaka huu, saa mbili asubuhi
katika Mtaa wa Ikulu, Kijiji cha Hogolo, Kata ya Hogolo, Tarafa ya
Zoisa, wilayani Kongwa. “Uchunguzi wa awali unaonesha chanzo cha
mauaji haya ni wivu wa mapenzi kwani marehemu alikuwa amevunja uhusiano
na mpenzi wake wa muda mrefu na kuanzisha uhusiano na kijana mwingine. “Hivi
sasa tunawashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji hayana ili
kufanikisha uchunguzi wa awali, tunamshikilia mpenzi mpya wa marehemu,
yule wa zamani hajulikani alipo baada ya kukimbia,” alisema Kamanda
Stephen.
Alisema katika tukio hilo, kaka wa marehemu ambaye anashikiliwa na jeshi hilo alidai kusikia purukushani zikitokea usiku wa tukio lakini hakuweza kutoka usiku nje ili kuangalia kilichotokea. Kamanda Stephen alisema marehemu alikuwa akiishi na babu pamoja na bibi yake ambapo siku ya tukio hawakuwepo nyumbani walikuwa katika vijiji jirani. “Bibi wa marehemu alikuwa Kongwa ambako alikwenda kujenga makaburi na babu yake alikuwa Kijiji cha Banyi Banyi ambako alikwenda kutemebelea wagonjwa,” alisema

Chanzo: Luppy Kung’alo, Jeshi la Polisi Dodoma (majira)
0 comments:
Post a Comment
Asante kwa kusoma habari hii! Tafadhali acha tupia maoni yako HAPA!