Subscribe:

Ads 468x60px

Labels

HII NI BIASHARA AU NI KWELI?..


Mbuzi aka Buzi la  la ajabu lijulikanalo kwa jina la ‘Mawimbi’ linafanya vitu ambavyo kwa akili za kibinadamu unaweza usiamini.

Buzi hilo linalomilikiwa na mr. Mawimbi mkazi wa Mazizini Ukonga, Bongo city karibu na Kituo cha Polisi Mazizini limeonekana kuwa kivutio kwa watu wa eneo hilo kutokana na kufanya vitendo vya kibinadamu.

Cops alitimba Mawimbi katikati ya wiki, nyumbani kwake hapo na kufanikiwa kuchonga na mmiliki/ shkaji lake la karibu ambaye alikiri mbuzi huyo kuwa na mashkolo kibao.

Mbuzi hujulikana kwa kula majani, lakini ‘Mawimbi’ yeye anapenda kula maraha az bibi bombaz vyakula kama nyama choma, nyama iliyopikwa, maandazi, chapati kwa mchuzi, ubwabwa kwa nyama, ugali, chipsi kavu na mihogo ya kukaanga ndiyo.

Muda mchache mr Mawimbi aliagiza watazamaji waliopiga hodi nyumbani kwake kwenda panapouzwa mapochopocho na kununua chapati ili waamini kile anachokisema juu ya buzi hilo mwenye uzito wa kilo 128.

Maajabu yake hayajaishia hapo tu, Mawimbi aliongeza kuwa mnyama huyo anakata kilevi kama hana akili nzuri. Alisema amekuwa akinywa aina zote za bia na ana uwezo wa kunywa za baridi zaidi ya 18 kutokana na uhitaji wake kwa siku bila kupepesuka wala kuwa bwii.

Swali lilikuja pale ambapo jamaa anajuaje kama mbuzi wake ana kiu ya bia?


Julius Mawimbi Kisena ‘Mawimbi’ akiwa na mbuzi wake wa ajabu.…


“Mara nyingi akipata hamu ya bia huenda kwenye baa na kuzungukazunguka hapo mpaka atakapohudumiwa.

Kama akiwakuta watu wanakunywa huwasogelea na kuwaangalia kwa macho yenye uhitaji. Wanaomfahamu humnunulia na kumwekea kwenye chombo na kumpa. Wasipotekeleza hilo hufanya fujo kwa kupiga kichwa meza za wateja mpaka kuangusha vinywaji vyao, 

Kila kizuri kina kasoro, wakati mbuzi huyo analeta mshangao kutokana na tabia yake hiyo lakini kumbe ana tabia za kubaka wanawake, hasa wale walio kwenye siku zao.Tatizo la mbuzi huyu ana tabia ya kubaka wanawake, hasa wale walioko kwenye siku zao, hadi sasa ana kesi 18 za kubaka katika Kituo cha Polisi cha Mazizini. Waathirika wakubwa ni wanawake hao ambao hupita karibu yake.
“Yeye akishasikia harufu ya mwanamke tu huanza kumkimbiza kwa lengo la kupata mambo ya kiutu uzima.

Hili nalo, Mawimbi analisimulia kama maajabu mengine ya mbuzi wake, kwamba alishawahi kuibwa mara 3 bila mafanikio kwani wezi hao walimrudisha wenyewe baada ya kuelemewa na uzito wake kama wa tembo. Anasema hata akiibwa kwa kuingizwa kwenye gari huwa mzito.

“Wamejaribu kumuiba mara 3 bila mafanikio. Kuna watu kwa nyakati tofauti walifanikiwa kumuiba na kumuweka kwenye gari lakini walishindwa kuondoka naye kutokana na kuelemewa na uzito.

Kutokana na hali hiyo, walimrejesha wenyewe na kuondoka zao. Kuna mwingine siku moja alikata bati kwenye banda na kutaka kuondoka naye lakini mbuzi alimpiga kwa pembe yule mwizi, asubuhi tukamkuta amepoteza fahamu, nikampa shilingi 2000 kwa ajili ya kwenda kujitibu maana aliumia vibaya,” alisema Mawimbi.
Mbuzi aka BUZI la Ajabu.
Mbuzi huyo ambaye amekuwa gumzo pande hizo aligongwa na pikipiki na kuvunjika mguu wa kushoto mbele. Mawimbi anasema alimfuata daktari wa mifupa wa Hospitali ya Amana ambaye alimfunga bandeji ngumu ‘P.O.P’ Kwa sasa mbuzi wangu hana raha, ana maumivu makali kwani hivi karibuni aligongwa na pikipiki, nikamwita daktari wa mifupa pale Amana, akaja akamtibu kwa kumfunga P.O.P, naamini Mungu atamsaidia kupona,” alisema.

 Mawimbi anakanusha madai kwamba maajabu ya mbuzi huyo hayatokani na mambo ya kishirikina, bali ni uwezo alionao kutoka kwa Mungu.

“Si mbuzi wa uchawi, ila ni mambo ya Mwenyezi Mungu tu,” aliweka wazi Mawimbi huku akiagana na waandishi. Gossip alichoka pale!

0 comments:

Post a Comment

Asante kwa kusoma habari hii! Tafadhali acha tupia maoni yako HAPA!