Mabibi na mabwana lazima tujifunze kitu kikubwa sana katika maisha haya ya watoto wetu na vijana kwa ujumla hasa wale wanaosoma ADHABU
ya viboko kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari nchini
inayotolewa na walimu na kuibua malalamiko miongoni mwa wazazi na
walezi, haijafutwa kisheria, imeelezwa.
Hayo
yamebainishwa na Ofisa Elimu Taaluma Mkoa wa Rukwa, Albert Mloka kwenye
mkutano wa wadau wa elimu uliondaliwa na Halmashauri ya Wilaya ya
Sumbawanga uliofanyika katika Shule ya Sekondari ya Matai wilayani
humo.
Mloka
alisema adhabu ya viboko shuleni imekuwa ikilaumiwa na wananchi wengi
nchini kwa kuwa walimu katika kuadhibu, hawachapi viboko, bali wanapiga wanafunzi kwa mateke, viboko visivyo na idadi, ngumi na vichwa.
“Kinachofanyika shuleni walimu wanakiuka taratibu na sheria zilizoainishwa na Serikali ambapo mbali ya kuwapiga
viboko visivyo na idadi kwa wanafunzi wakosefu, lakini pia walimu wa
kiume wanawapiga wanafunzi wa kike ambapo sheria haisemi hivyo,” alifafanua Ofisa Elimu wa Mkoa.
Alisema
mwanafunzi ataadhibiwa kuchapwa viboko pale itakapobainika kuwa kosa
alilofanya ni ovu na adhabu yake ni viboko au kufukuzwa shule na si
vinginevyo.
Kuhusu viboko kwa wasichana, alisema wataadhibiwa
kwa kuchapwa viboko na walimu wa kike pekee kama shule haina mwalimu wa
kike, basi adhabu hiyo itatolewa na Mkuu wa Shule na Mwalimu Mkuu.
Alisema ni viboko vinne tu vilivyoruhusiwa kisheria kwa wavulana kuchapwa kwenye makalio
na wasichana mikononi na mwalimu akitoa adhabu hiyo, anaagizwa aandike
kitabuni kuonesha tarehe na idadi ya viboko na aliyeadhibiwa lazima
asaini kitabuni humo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Daniel ole Njoolay aliwavunja mbavu wajumbe alipochangia kwa
kusema kuwa “mbona sisi (wanafunzi wa kiume) tunachapwa na walimu wa
kike…this is not fair, mie ni Mmasai kule umasaini mtoto wa kiume
kucharazwa viboko na mwalimu wa kike looh mwalimu huyo atapewa
misukosuko kwa kweli atapata shida,” alisema.
Wajumbe
wengi wakichangia walidai kuwa walimu wanaotoa adhabu ya viboko visivyo
na idadi shuleni hata kwa kosa la mwanafunzi kushindwa kujibu swali
darasani, wengi wao hawana uwezo wa kutosha kufundisha au hawajiandai
vizuri kufundisha.
“Si
kweli shule zimeharibika, bali walimu baadhi yao wameharibika....viboko
sio suluhisho la kumaliza utoro shuleni, walimu wanaotembea na fimbo
mikononi kutwa nzima basi ujue wewe si mwalimu,” alisema mjumbe mmoja.
Wajumbe
hao pia walishauri kuwa adhabu hiyo ya viboko kwa wanafunzi kamwe
isitolewe na mwalimu mwenye hasira kwani atapiga badala ya kuchapa.
Baadhi
ya wanafunzi ya Shule ya Sekondari ya Matai walioalikwa hapo, walikiri
kuwa adhabu za viboko shuleni zimekithiri na ni mateso kwao.
“Maisha
ya shule yamekuwa ni mateso kwetu kwani adhabu za viboko zimezidi
baadhi yetu wamekata tamaa ya kusoma na wanahudhuria shule kwa lazima na
si kwa hiyari yao wenyewe” alisema mwanafunzi wa kidato cha nne, Paulo
Maembe.
Chanzo: Habari Leo.
- Kwingineko, wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Rungwa katika Halmashauri ya Mji wa Mpanda wamegoma kuingia madarasani kwa muda usiojulikana wakipinga Mkuu wa Shule hiyo kuwacharaza viboko visivyo na idadi. Kwa habari kamili soma HAPA.
0 comments:
Post a Comment
Asante kwa kusoma habari hii! Tafadhali acha tupia maoni yako HAPA!