Picha hii iko HAPA
- Kama ulisomea Tanzania hasa katika shule za serikali bila shaka utakuwa bado unawakumbuka wale walimu waliokuwa wakisifika kwa kutembeza viboko. Ukichelewa shuleni, unaambulia viboko. Ukiwa hujafua nguo, kukata kucha, kuchana nywele, kusugua meno au kukoga unaambulia viboko. Ukizungumza darasani, viboko. Ukiulizwa swali na mwalimu halafu ukaboronga jibu ni viboko. Ukitoroka shuleni viboko tu. Viboko vilikuwa kila mahali na kama ulikuwa na siku yenye balaa basi mtu ungejikuta jioni inapoingia tayari unakuwa umeshaambulia viboko zaidi ya kumi. Na ukifika nyumbani napo unaweza pia ukaambulia viboko. Viboko !
- Kwa sasa ukikaa na kufikiri vizuri, unaionaje adhabu ya viboko? Ilikusaidia kuwa na adabu njema, kuzingatia masomo na hatimaye kuwa mwanafunzi mzuri na mwanajamii mwenye manufaa; au adhabu hiyo ilikufanya uwe sugu na mtu asiyejali? Ni sawa kuwapiga watoto viboko? Unaunga harakati za kuifuta adhabu hii mashuleni?
- Tafiti mbalimbali kutoka nchi za Kimagharibi zinaonyesha kwamba viboko na adhabu zingine zenye kuleta maumivu hazisaidii cho chote na zinaweza kuwafanya watoto kuwa na tabia mbaya na wasiojali. Ndiyo maana katika nchi nyingi za Kimagharibi, adhabu ya viboko imeshapigwa marufuku. Tafiti kama hizi ni kweli zinaakisi hali halisi katika mazingira yetu na malezi ya Kiafrika? Tufute viboko mashuleni?
*********
0 comments:
Post a Comment
Asante kwa kusoma habari hii! Tafadhali acha tupia maoni yako HAPA!