Subscribe:

Ads 468x60px

Labels

INAKUAJE NEEMA ANIDISS MIMI?

"Simjui huyo Ney ni nani anaigiza filamu au ni demu gani? Alihoji Afande Sele then akaendelea kwa kusema, "mimi najua  majina kama hayo ni ya mademu sasa iweje Neema anidiss mimi?"
Ni kauli ya  nyota mwenye 'Crown' ya mkali wa Rhymes nchini Seleman Msindi 'Afande Sele'  alipokuwa akizungumza na mtandao unaomilikiwa na media kubwa ya Clouds Entertainment Teentz.com kuhusiana na 'diss' dhidi yake iliyotolewa na  msanii mwenye uwezo mkubwa wa kuchana hivi sasa hapa Bongo, Ney wa Mitego kupitia  track yake mpya  iliyopewa jina la 'Nasema  Nao'.
Akizungumza na mtandao huo namba moja kwa habari za mastaa, Afande Sele mwenye maskani yake  pande za  Morogoro mji kasoro bahari amesema kuwa kamwe hajawahi kusikia  wala kujua kama  kuna msanii wa hip hop hapa Bongo anayeitwa Ney na kusisisitiza kuwa hamjui huyo mtu kabisa.
Alipotakiwa kusema kama ameisikia Track hiyo Sele  alifunguka  kuwa  hajui kitu chochote kuhusu wimbo huo na anaamini kuwa hakuna wimbo wa  Hip hop ulitolewa hivi karibuni.
"Binafsi sijaisikia na sijui lolote, nitajaribu kufuatilia, nitaitafuta track hiyo niisikilize na kama atakuwa amefanya hivyo basi nitamlinganisha na mtu anayemtukana Usain Bolt halafu akaanza kukimbia  alisema Sele.
Tuache bifu za ki****** maze huu ni muda sasa wa kufanya bifu na serikali yenu isiyo na msimamo na kuachia chakula kikapanda bila formula! Kueni na bifu na pesa sio udandara unaoendelea Nchini, halafuuu by the way, wasanii ndo kioo cha jamii mkifanya hivyo mnataka muwe aje? vyombo vya habari vireport utahira wenu siyo?...

0 comments:

Post a Comment

Asante kwa kusoma habari hii! Tafadhali acha tupia maoni yako HAPA!