“MOYO wangu umegandwa na mavumbi, macho yamepofuka kwa machozi, kwani mateso
yangu hayapimiki kwa mizani, kila mtu ananihukumu kwa uongo na hadithi za
kutunga juu ya ndoa yangu pasipo kujua ukweli,” ndivyo anavyoanza kusimulia
staa wa filamu za Kibongo, Halima Yahya ‘Davina’ akielezea wakati mgumu
anaokutana nao baada ya kuwepo na mgogoro kwenye ndoa yake.
Akaeleza kuwa, siri za ndoa huzijua wahusika na kwamba hata yeye kufikia hatua ya kutengana na mumewe anajua chanzo ni nini na si rahisi kumueleza hata mama yake mzazi, ila watu wanatumia maneno makali yanayomuumiza.
“Kila mtu anasema analolijua, hakuna aliyenilazimisha kuolewa, kilichonifarakanisha na mume wangu tunakijua sisi wawili (yeye na mumewe), labda na watu wangu wa karibu, lakini kwa sasa maneno yamekuwa mengi sana, tena yenye kuumiza kiasi kwamba kuna wakati natamani hata kujitoa uhai.
Chanzo: Bongomovies
0 comments:
Post a Comment
Asante kwa kusoma habari hii! Tafadhali acha tupia maoni yako HAPA!