Leo nilipata nafasi ya
kuzingumza na Gadan G Habash ambaye ni Meneja na Mume wa Mwanamuziki maarufu
nchin Lady Jay Dee, sote tunafahamu juu ya maneno aliyoyasema Lady Jay Dee kama
ni Wosia wake.
Kupitia kipindi cha The Takeover kinachorushwa na
kituo cha TBC fm haya ndio yalikuwa majibu ya maswali niliyomuuliza Gada G;
Ipi ni Kauli yako juu ya Wosia wa Lady Jay Dee...?
Gadna G: Ni maneno ambayo yametoka moyoni
mwake na ni maneno mbayo anajitetea kama msanii, mimi kama
Meneja ukiacha pia kama mke wangu naendelea kumsapot kwa kile ambacho
anaona ni sawa, basi mimi nitaendelea kumsaport na kujaribu kuzungumza na
Lady Jay Dee, mara nyingi anasema tu kwamba watu wasifikilie ni swala la
wimbo kupigwa au kutokupigwa, hayo ni mambo ya kawaida lakini wafikirie tu
kwamba huyu mtu anaongea kutokana experience yake aliyokuwa nayo na wale watu.
Baada ya mwaka 2003 kuacha kufanya kazi kwenye
management yao ya Smooth Vibe, yalitokea mambo mengi hapa katikati ila
hakusema lakini siku za hivi siku za karibuni kuna mengine ambayo yametokea,
ndio akaona hapana nisipo sema nitazidi kukandamizwa na matokeo yake nitakufa
kisabuni.
Hii ni kama vita mmejipangaje..?
Gadna G: Unapoamua kusema ukweli swala la
kujipanga mara mbili huwa halipo, ni kwamba unasema ukweli watu wasikie
naukizungumzia uhasama watu watauliza juu ya uhasama lakini ulikuwepo
tayari kwahiyo tu watu wanajua kwa sasa kwa kuwa jdee ameamuwa kuongea lakini
tu hawajui tu kwamba jdee alikuwa na matatizo na wale watu tangu kipindi cha
nyuma sababu wale watu wanafumo dume ya kufanya kazi na alipoachananao aliona
kama wanamfatilia kulekule ambapo yeye alipo
Nini mlikiona kama chokochoko...?
Gadna G: Unajua kwa mfano unaweza kumuomba mtu
maji akakwambia sina, ukayaona yale pale ukamwambia niuzie akakuuzia ila
bado alivyokuuzia akaona kama unafaidi, mwisho akakwambia yameisha
nenda sehemu nyingine, ukaenda sehemu nyingine na ukayapata bure, akaona
umepata akaamua kukufata kulekule na akakukuta unakunywa maji kwenye grasi
kisha akakuputa, sasa hapo inabidi useme hapa unavyofanya sio sawa ndo hicho
anachofanya Jay Dee sasa hivi.
Hali hii imewaathiri kwa kiasi gani...?
Gadna G: Cha kushukuru Mungu ni kwamba
msanii au hata pia stesheni ya redio inategamea umma wa Watanzania au
hata mashabiki kwa ujumla kwa kuwepo kwake.
Jay Dee anapata saport nzuri kutoka
Watanzania, basi ujue hata hajaathirika chochote, na pia tu anaendelea kufanya
kazi kwa bidii, ila tu isipokuwa unapoona mtu anafanya madhara ili tu mtu apate
athari fulani ndio unasimama kuongea, ndiyo maana tuna Bunge na watu
wanasimama, watu wanaongea, watu wanatetea hoja, ndiyo maana yake. Yani lazima
mtu usimame useme ukweli kwa unalohisi hili jambo litanipa madhara nisiposema.
Gadna G: Uwoga ni kitu ambacho binadamu
tumeumbiwa, wakati mwingine unasaidia wakati mwingine unakudhiru uwoga wako,kwa
sababu wanasema adui wa maendeleo yako mwenyewe ni wewe mwenyewe, ndiyo maana
uwoga wako unaeza ukasabishwa ukakandamizwa zaidi, ndiyo maana wazee wetu
waliweza kusimama na kuikomboa hii nchi kwa sababu walisimama hawakuogopa.
Wangeogopa hii leo hii nchi tusingekuwa huru, kwa hiyo kama kuna mtu ana jambo
na anaogopa kusema hilo ni jambo la kawaida kuogopa, lakini wakati wa kusema
ukifika usiogope kusema ili mradi useme ukweli, basi inatosha....
Kauli yako ya mwisho ni ipi..?
Gadna G: Ni kwamba wanahitaji kujua ukweli na
kuambiwa ukweli, mtu yoyote anayejua kitu cha kweli anaweza kusema sio
sawa, utaendelea kukandamizwa. Kauli ya mwisho ndo hiyo wanahitaji
kuambiwa ukweli na kusikia ukweli ili kama wanakosea wasiendelee
kukosea wabadilikee….
AKIONGEA NA MTANGAZAJI DAN CHIBO MTANGAZAJI
WA TBC FM,NA HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA
0 comments:
Post a Comment
Asante kwa kusoma habari hii! Tafadhali acha tupia maoni yako HAPA!