MANEKY PRODUCER WA AM RECORDS |
Wakati wimbo wa Diamond ‘nataka kulewa’ ukitengeneza topic kwenye media kibao TZ na kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ambapo wengi wanasema beat hiyo inafanana asilimia 100 na ile ya beat ya wimbo wa Pasha alomshirikisha Tunda Man ‘Mtoto Amekua’, Manecky wa AM records ambaye ndiye aliyetengeneza ‘nataka kulewa’ amesema beat ya wimbo huo ni tofauti kabisa na ile ya wimbo wa Pasha.
Producer huyo ambae ndiye mshindi wa kili music awards 2011 kama producer bora wa mwaka alifunguka kwa msisitizo kwenye kipindi cha XXL cha Clouds fm kuwa hakusample beat sehemu yeyote ile na hiyo beat aliifanya kwa mawazo yake mwenyewe kuanzia mwanzo kabisa.
Alipoulizwa maoni yake kama beat hizo mbili zinafanana au hazifanani, alisema “kwa kitu ambacho mimi nimeweza kusikiliza hizi ni beat mbili tofauti, sema kuna idea ya lead sound ambayo inaweza kuwa na mfanano flani, ndio maana nikarudia kusema palepale, mimi ni mtu ambae nasikiliza muziki kila siku, na ni binadamu na sio computer sio kitu flani ambacho kinasema ni kitu flani kifanye hivi…!”
Manecky amesema hata Tunda Man aliisikiliza ‘beat ya Nataka kulewa’ mara nyingi tu lakini hakuweza kuifananisha kabisa na ile ya wimbo wa Pasha ambayo yeye mwenyewe kaweka vocal zake kwenye, lakini inaonekana alipousikia watu wanasema zinafanana ndipo na yeye akashtukia kuwa inawezekana iko hivyo..
Kweli tunatofautiana kushtukia copy, wengine wakisikia hata kinanda cha kwanza tu wanashtukia ila Tunda Man yeye ameshtuka baadae sana pamoja na kuitumia beat hiyo.
Cover matata iliyotengenezwa chini ya mikono ya wanaojua kazi zao! I-View Studios chini ya Mkubwa RAQEY MOHAMED bwana MENEJA. |
Ushauri! Ni bora kuziachia ngoma zote on air ili wanajamii tuweze kuzihukumu wenyewe! haitasaidia tuking'ang'ania kuwa DIAMOND ameiba wimbo mara ameiba Beat! aaaaaa hayo ni maneno ya uoga tena ni uoga wa hali ya juu! wasanii acheni hofu achieni nyimbo zenu! ili tuzichanganue.. ni hayo tu! ninyi nyote ni STARZ ilaaaaa....
0 comments:
Post a Comment
Asante kwa kusoma habari hii! Tafadhali acha tupia maoni yako HAPA!