Subscribe:

Ads 468x60px

Labels

KUNA NJIA YA KUPUNGUZA UFISADI NCHINI!

Picha hii inapatikana hapa
  • Ufisadi - tatizo sugu na hatari linalodidimiza maendeleo ya Afrika kumbe linaweza kupunguzwa kwa kutumia njia rahisi tu. Utafiti uliofanywa na Benki ya Dunia unaonyesha kwamba serikali zenye wanawake wengi madarakani (mf. Wabunge, Mawaziri) zina viwango vidogo vya ufisadi ukilinganisha na zile zilizosheheni wanaume. Rwanda - nchi ambayo inaongoza duniani kwa kuwa na wanawake wengi bungeni na serikalini inatajwa sana kuwa mfano wa kuvutia kuhusu suala hili. Ni kwa sababu hii kujitokeza kwa wanawake wengi kugombea ubunge na uwakilishi kule Haiti katika uchaguzi wa mwaka huu kumeleta matumaini makubwa kwamba pengine ufisadi utapungua.
  • Tafiti mbalimbali zimeonyesha kwamba wanawake wana huruma kuliko wanaume, wana moyo wa kujinyima, wanaaminika zaidi na ni wepesi wa kuona na kukiri makosa na hatimaye kuomba msamaha. Pengine ni kutokana na sababu hizi wanawake pia wana uwezekano mdogo wa kuiba mamilioni ya pesa za umma na kuwaacha wananchi wanyonge wakiteseka (wengi wao wanawake wenzao; na watoto). 
  • Serikali zenye wanawake wengi madarakani pia zina uwezekano mkubwa zaidi wa kuendeleza sera imara zenye kumakinikia sekta za afya na elimu ya watoto, usawa kwa wanajamii wote na kuendeleza uchumi imara.
  • Pengine nasi inabidi tuige mfano wa Rwanda ili tuone kama visa vya ufisadi vitapungua. Utafiti huu wa Benki ya Dunia unapatikana hapa.

0 comments:

Post a Comment

Asante kwa kusoma habari hii! Tafadhali acha tupia maoni yako HAPA!