Dk.
Steven Ulimboka aerejea nchini na kutoa shukrani za dhati kwa
watanzania wote kwa dua na michango yao ya dhati kuinusuru afya yake na kuahidi
kuendeleza mapambano dhidi ya huduma bora za afya na maslahi kwa
madaktari.
Ulimboka
amerejea nchini wakati jamii bado ikiwa katika kizungu mkuti cha nani
hasa aliyemteka na kumpa mateso makali Dk. Steven Ulimboka ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini na kiu ya wananchi sasa ni
kutaka kujua ukweli kupitia kwake.
Daktari
huyo ambaye amejizolea umaarufu nchini kwa harakati za kudai haki na
maslahi ya madkatari na huduma bora Hospitalini amerejea leo August 12, 2012 jijini Dar
es Salaam akitokea nchini Afrika kusini ambako alipelekwa na Madaktari
wenzake tangu Juni 30 mwaka ambako alikuwa akitibiwa majeraha
aliyoyapata baada ya kutekwa na kundi la watu wasiojulikana.
Dk.
Ulimboka alitekwa, kupigwa na kutelekezwa kwenye Msitu wa Pande nje
kidogo ya jiji la Dar es Salaam ambapo Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya
Dar es salaa lilidai kuwa aliyemteka daktari huyo ni raia wa Kenya
ambaye tayari wanamshikilia.
Dk.
Ulimboka amewasili leo majiya ya saa 8 alasiri katika Uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na SA Airways
na kulakiwa kwa shangwe, hoihoi nderemo na vifijo kutoka kwa ndfugu
jamaa na marafiki sambamba na madaktari wenzake na wanaharakati.
Hakika
Mungu yupo! Na anatenda miujiza yake, Ulimboka inakumbukwa aliondoka
nchini akiwa hajiwezi kutokana na hali yake kuwa mbaya na kubebwa katika
machela lakini leo amerejea mzima wa afya na anatembea mwenyewe.
Licha
ya vurugu za hapa napale ambazo zilikuwa zikisababishwa na ndugu na
jamaa ambao walitaka wanahabari wasilidake tukio hilo la kihistoria
mithili ya Mtanzania kutwaa medali ya Dhahabu Olympic 2012 huko London
lakini paparaziu waliweza kunasa taswira kadhaa na kuongea nae.
“Nimepona
ndugu zangu….nawashukuru nyote mlioniombea, watanzania, madaktari,
ndugu na jamaa zangu nashukuru pia kunisaidia kupata matibabu bora hadi
leo hii narudi nyumbani, niko fiti nikitembea mwenyewe,” alisema Dk.
Ulimboka.
Miongoni
mwa wana harakati ambao Father Kidevu Blog ilifanikiwa kuwaona uwanjani
hapo ni pamoja na Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Usu
Malya na Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari wanawake(TAMWA),
Ananileya Nkya.
Wanaharakati
hao walijipamba na mabango kadhaa yaliyo kuwa na jumbe za “Dk Ulimboka
karibu nyumbani uliumizwa kikatili ukitetea afya bora kwa watanzania.”
“Dk Ulimboka damu yako ilimwagika na kuamsha ari kwa wananchi kudai
huduma bora za afya.” “Dk Ulimboka wewe ni mpigania haki na afya bora
kwa wananchi wote Mungu na watanzania wote tuko nawe.”
Nae
Katibu wa Jumuiya hiyo Dk. Edwin Chitage ameiambia father Kidevu Blog
kuwa kurejea kwa Dk. Ulimboka akiwa mzima ni ishara ya huduma bora
aliyoipata akiwa nje ya nchi.
Usiku
wa kuamkia Juni 27, 2012 watu wasiofahamika walimteka, kumpiga, kumng’oa
kucha na meno kisha kumtelekeza kwenye msitu wa pande Dk. Ulimboka.
Wakati
amelazwa Hospitali ya taifa Muhimbili chumba cha wagonjwa mahututi
Kitengo cha Mifupa (MOI) alikuwa akihudumiwa na jopo la madaktari saba
akiwapo Profesa Joseph Kahamba.
Licha
ya jopo jilo la madaktari kumhudumia kwa ukaribu lakini walishindwa
kupata baadhi ya vipimo ili kubaini iwapo damu yake ilikua na sumu ama
la kwa kusababu baadhi ya dawa zilishindwa kufanyakazi ndfipo uamuzi wa
haraka wa kumpeleka nje ya nchi ukafikiwa na wanachi kumchangia fedha
kiasi cha shilingi milioni 40 za matibabu yake.
Aidha
Katibu wa Jumuia ya madaktari Dk. Chitage amewaahidi wanahabari kuitisha
mkutano mapema ili kujuza umma wa watanzania na dunia kwa kina kuhusu
kupona Dk. Ulimboka.
0 comments:
Post a Comment
Asante kwa kusoma habari hii! Tafadhali acha tupia maoni yako HAPA!