Mfanyabiashara mashuhuri wa mjini Moshi, (jina linahifadhiwa)
ameingia katika kashfa nzito baada ya kurekodi mkanda wa video
ukimwonyesha akimlawiti mfanyakazi wake wa dukani.
Kifungu namba 154 cha kanuni ya adhabu kimeweka
adhabu ya kifungo cha maisha kwa mtu anayepatikana na hatia ya kufanya
mapenzi na mtu mwingine kinyume cha maumbile.
Video za mfanyabiashara huyo ambazo zimekuwa gumzo
zimekuwa zikisambazwa kupitia mitandao ya simu hususan Whatsapp na
nyingine zikiuzwa katika maduka yaliyopo Stendi Kuu ya Mabasi Moshi.
Inadaiwa kuwa mfanyabiashara huyo kijana
anayemiliki maduka matatu Stendi Kuu ya Mabasi, alirekodi video hizo kwa
siri bila mfanyakazi wake huyo kujua na kuihifadhi kwenye kompyuta.
Haijajulikana ni nani aliyeingia katika kompyuta
hiyo na kunakili picha hizo ambazo moja ina sekunde 45 na nyingine
inayomuonyesha akimlawiti mfanyakazi wake huyo ikiwa na muda wa dakika
nane.
Habari za uhakika zilizopatikana zimedai kuwa kwa sasa mfanyabiashara huyo pamoja na mwanamke huyo
wametoroka na hawajulikani walipo baada ya kubaini wanasakwa na polisi.
Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Robert Boaz
alipoulizwa jana alisema ingawa hajaona video hizo, lakini kufanya
mapenzi kinyume cha maumbile ni kosa la jinai hivyo watamtafuta
mfanyabiashara huyo.
Kamanda Boaz alisema polisi wanamsaka ili ahojiwe
kuhusiana na video na vitendo hivyo alivyoiita ni vichafu na kwamba
kimsingi anatakiwa kujisalimisha mwenyewe ili kumaliza mambo.
Alitoa wito kwa jamii kufuata maadili ya dini zote ambapo zinawataka binadamu waishi kwa kumtii Mwenyezi Mungu.
source: freebongo
0 comments:
Post a Comment
Asante kwa kusoma habari hii! Tafadhali acha tupia maoni yako HAPA!