Msanii mkongwe na maarufu nchini, Juma Kassin
Kiroboto, aka Nature, ameonyesha kukerwa na kile kilichoendelea jana usiku
katika kipindi cha burudani cha televishen inayotizamwa africa ya
mashariki alipokuwa akifanya nao interview. Nature alionekana akiwa amevaa
kawosh na ndala na mara baada ya mahojiano mafupi ya mwanzo ambapo mtangazaji
alisema watarejea baada ya mapumziko mafupi Nature hakuonekana tena.
Kilichotokea kwa mujibu wa Nature mwenyewe, ni wakati wa mapumziko hayo,
mtangazaji wa kipindi hicho alimfata na kumuambia kuwa hataendelea na interview
tena kwasababu ya mavazi aliyokuwa kavaa ambayo ni ndala na kawosh. kuonyesha
kukerwa kwake na ishu hiyo Nature aliamua kuandika kupitia ukurasa wake wa
facebook....
hivi kwa mfano
angekuwepo mzungu pale na kavaa ndala wangesitisha mahojiano na kuvaa kaoshi ni
tatizo,kunywa nimekunywa bt kuna baya nimeliongea na hivi kama kweri we
nimuandishi wa habari unaruhusiwa kuvaa vile kisheria kama yule mtangazaji
nimeboreka kinoma na ikiwezekana nasitisha kuanzia ssa kupeleka ngoma zangu
pale siitaji interview
0 comments:
Post a Comment
Asante kwa kusoma habari hii! Tafadhali acha tupia maoni yako HAPA!