Subscribe:

Ads 468x60px

Labels

BEKA IBROZAMA ALMASI ILIYODONDOKA TOKA MIKONONI MWA THT


Baada ya BEKA kuondoka THT maneno mengi sana yamesemwa mara hivi, mara vile kila mtu akihisi lake kuhusiana na BEKA IBROZAMA kijana mtanashati kinara aliyevuma sana ndani ya shule ya muziki ya THT, baada ya kimya kingi sasa Beka Ibrozama aamua kufunguka mwenyewe, “Sijaondoka THT kwa sababu nyingi za kuhisi! Kwanza ningependa wadau na mashabiki wa muziki wa Bongo flavor wafahamu kuwa najivunia sana kupitia shule ya muziki yenye bahati ya kuwa na walimu wasomi wanaouelewa muziki vema! Kikweli najivunia sana kuwa mmoja wa mwanafamilia wa THT, sababu gani nimeondoka THT hilo ndo swali la msingi!! Well, kwanza ni lazima wadau waelewe kuwa THT ni sehemu ya kujifunzia muziki! Na mimi nilienda pale kupata vitu zaidi kwa wanaoufahamu muziki kiundani hivyo muda niliokaa chuoni kumenifanya niive vyema katika uimbaji! unajua, THT ni kama baba! Sisi ni kama wana, mwana anapoishi katika familia yenye watoto wengi akishakuwa kipimo cha yeye kuweza kujitegemea  huwa anatoka kwa baba na kwenda kujitafutia maisha kwa majaribio, mimi nilikuwepo kwa baba nimetoka najitafutia, na sio kwamba nipatapo tabu mahali nitasita kumfuata baba na kumueleza panaponipa tabu NOO!! Nitarudi nyumbani na kuomba ushauri ni njia gani naweza kutatua tatizo langu!” alisema BEKA mwana wa IBROZAMA mr. Manywele.

Hata hivyo kuna kitu cha tofauti kidogo kimejitokeza kwa BEKA IBROZAMA katika muonekano wake! Hivi karibuni Beka ameonekana kuwa na muonekano mpya wa nywele zake ambao umebadilisha kabisa muonekano wake kwa kiasi kikubwa sana Beka amesema katika sanaa hususani ya muziki na maigizo/filamu kuna kitu kidogo sana kinaweza kukubadilisha ili uonekane wa tofauti! Unajua, ni lazima kila mtu awe mbunifu kwa kila kitu anachokifanya! Kwa mfano mimi zamani nilikuwa nikipita mahali ilikuw sio rahisi watu kujua kama BEKA amepita kwa kuwa nilikuwa sina tofauti na watu wa kawaida wale wasiokuwa wanasanaa. Ila kwa sasa namshukuru Mungu kila napopita watu hunishangaa na kupata urahisi wa kufahamu kuwa Yule ni BEKA, nakuhakikishia hata kama mtu yupo nyuma yangu atajifanya anakimbia ili akifika mbele yangu ageuke aangalie kwani huyu ni nani? Ni jambo latofauti sana! Kiukweli namshukuru MUNGU kwa hilo.


Baada ya muhtasari sasa ni habari, nilijaribu kumdodosa dodosa BEKA kwanini ulikuwa kimya sana muda wote huo? Kukaa kwangu kimya muda mrefu nilikuwa nikisoma game linaendaje but nishajua likoje nachopenda kuwaambia mashabiki wangu kuwa mwaka 2013 nataka kuonyesha jinsi gani nauelewa muziki na vitu vingi katika tasnia hii ya muziki tofauti sana na wenzangu!

Ombi langu naomba wadau watupambanishe cc wasanii kwa wasanii tupate kujua nani anaweza na nani hawezi ili kuweka ushindani katika muziki wetu Tanzania. Alisema Beka, hata hivyo Beka aliwataka mashabiki zake wakae mkao wa kula, soon naingia kitaaani kwa spika za redio zenu na track mpya inayoitwa UNALIA NINI? baada ya NARUDI KAZINI. Nawapenda sana!

Sikusita kumpa nafasi ya kuwashukuru wale wote waliomfikisha hapo alipo, “Natoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa MUNGU wangu aliyeniumba na kunipatia pumzi na vipaji bure, pili nawashukuru wazazi wangu kwa kuthubutu kunipa nafasi ya kujaribu na kufanya Muziki! wale waliokuwa karibu na mimi kwa njia moja au nyingine kuhakikisha BEKA yupo hapa alipo, kwanza kabisa nimshukuru  H29487 mihayotheprince kwa kusimama vema kama manager wa BEKA na kufanikiwa kufanya yake, pili, napenda kumshukuru Mr. Hassan Apelee kwa kunipa ushauri mara zote napokuwa nahitaji kufanya lolote kwenye muziki na maisha! Tatu napenda kuwashukuru kwa dhati walimu wangu wote walionipiga msasa kwa kipindi chote nilichokuwa THT, kabla sijafika mwisho nashukuru uongozi mzima wa THT, Clouds MEDIA group na wafanyakazi wao wote kwa kumuonyesha BEKA njia ya Mafanikio. Napenda kuwashukuru watangazaji na Madj wote wa MEDIA zote nje na ndani ya nchi ya TANZANIA wanaohusika kumfanya Beka akasikika na kupendeka kwa mashabiki zake! Siwezi kuwasahau wapishi maproducer wa BEKA Ibrozama, asanteni sana, Last nawashukuru sana mashabiki zangu kwa kunipokea na kunifanya niwe juu zaidi yao. Eleweni ninyi ni wa muhimu sana kwani hakuna BEKA bila ninyi so NAWAPENDA SANA, tena sana! Mung awabariki sana.

0 comments:

Post a Comment

Asante kwa kusoma habari hii! Tafadhali acha tupia maoni yako HAPA!