MWIZI ANAPOMBWELA 40 HUFIKA.
Siku zote za maisha yetu huwa tunajaribu kumuhesabia kachaaa anayejifanya kidokozi wa mali za watu, so inapofikia 40 yake hapo ndipo anapopata chai yake! Pasipo kutegemea mwizi anapoiba na kujaribu kutafuta mambio ananaswa na wananchi wenye asira kali hapo ndipo kizazaaa kinapotokea! asipokabiliwa na kifo, basi mauti yanamuitaji, kama si mauti! basi hata joto ya jiwe tu! Ilaaaa Wananchi lazima tuwe makini na sheria mida mingine ijapokuwa na hawa wanausalama nao wanatuzingua!wakimshika mtu! end of day unakutana naye kitaaaani dats kill us for sure! kwa hiyo unapokutana na mdasi kanyaka mali ya watu na ukakumbuka kuwa kuna mmoja wa wadasi hao alikunyofolea chakwako, aaaaaa usintanie wewe hapo ndipo 40yake inapofikia! sasaaaaaaa...
Selaaa mmoja alipeleka picha hii mahala kwenye chombo kimoko cha habari then akasema huu si ustaarabu hata kidogo mimi nakubaliana naye nusu ila aaah tuendeleee, jamaaa akaendelea kusema kwamba jamaa alichomwa kwa kutuhumiwa wizi wa pikipiki. Alipiga picha nyingi na na kuna nyingine ambazo hazitamaniki hii ina nafuu nimeibadika kuwasilisha ombi la mleta habari kilichonga chombo hicho. Alisema kwamba polisi wa Kimara walifika eneo hilo muda mfupi kabla hajachomwa moto wakajiondokea ambapo wangeweza kuokoa maisha ya mtuhumiwa huyu.
Watu wamechukua sheria mkononi wameua na kumchoma moto mtu ambaye hana makosa kwa kudhani kwamba ameiba pikipiki wakati alikuwa ametumwa mafuta na fundi ambaye alikuwa anatengeneza pikipiki hiyo.
Tukio hili la kusikitisha limetokea siku chache zilizopita na mbaya zaidi nimeibandika kwenu japo haipendezi kuweka lalamiko la msomaji kwamba polisi hawakujitahidi kuzuia mauaji haya. Picha na Rahabu/Kimara
Blog ya jiachie imelaani na itazidi kulaani vikali vitendo ya namna hii vya kujichukulia sheria mkononi, ambavyo vimekuwa vikiibuka mara kwa mara ndani ya jamii yetu na kusababisha kupoteza uhai wa watu,Wanajamii tuachane na tabia hii ya kujichukulia sheria mkononi,Sheria zipo kwa ajili ya kulinda na kutetea haki ya kila mwanajamii,basi na itumike njia hiyo ya kufuata sheria.
Asante, nawakilisha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Asante kwa kusoma habari hii! Tafadhali acha tupia maoni yako HAPA!