Msanii
wa filamu nchini Tanzania aliyejaa vibweka na utanashati, mwanadafada Elizabeth Michael Kimemeta Mwenye umri usiojulikana, maarufu kama Lulu,
anayekabiliwa na tuhuma ya kesi ya mauaji ya msanii nguli aliyefahamika kama mpenzi wake wa siku nyingi marehemu Steven Kanumba, jumatatu ya tarehe 18, alirudishwa mahabusu bila kupanda kizimbani katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam hadi hapo
Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, itakapotoa uamuzi kuhusu
suala la utata wa umri wake.
Baada ya mshtakiwa huyo kufikishwa mahakama hapo jumatatu
hakupandishwa kizimbani kutokana na jalada la kesi hiyo kuwa Mahakama
Kuu, ambapo suala la utata wa umri wake litasikilizwa Juni 25, mwaka
huu mbele ya Jaji Dk. Fauz Twaib.
Lulu alirudishwa mahabusu kutokana na sheria kutoruhusu usikilizwaji wa awali kuendelea wakati Mahakama Kuu inaendelea kusikiliza maombi yaliyowasilishwa na mshtakiwa kutaka umri wake uchunguzwe.
Lulu alirudishwa mahabusu kutokana na sheria kutoruhusu usikilizwaji wa awali kuendelea wakati Mahakama Kuu inaendelea kusikiliza maombi yaliyowasilishwa na mshtakiwa kutaka umri wake uchunguzwe.
0 comments:
Post a Comment
Asante kwa kusoma habari hii! Tafadhali acha tupia maoni yako HAPA!