BAADHI
ya walimu wilayani Mbulu, Manyara, wameilaumu serikali kwa kuajiri
walimu wapya ambao wamekuwa wakijali zaidi maslahi binafsi badala ya
wito wa kuwafundisha. Wakizungumza
kwa nyakati tofauti na gazeti la watu Tanzania Daima wilayani hapo(Mbulu), walisema walimu
wanaoajiriwa hawapo tayari kufundisha masomo ya hisabati, Kiingereza na
Sayansi kwa kuwa hawana msingi mzuri.Mwalimu
Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Harka, Joseph Hando alisema kwa sasa
taaluma imechuja kwa kuwa walimu waliopo wapo kimaslahi zaidi.“Sehemu
kubwa ya walimu wa zamani ilikuwa ni kujitolea tofauti na ilivyo sasa,
walimu hao wamekuja kupata ajira tu. Taaluma nayo imechuja,” alisema
Hando.Naye
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Sanubaray, Debora Msuya,
alisema ufundishaji wa walimu wanaotoka vyuoni hivi sasa ambao
wanajulikana kama wa dot.com ni tatizo kwa kuwa wanaandaliwa kwa
kulipuliwa.Alisema
katika ufundishaji wa darasa la kwanza na la pili, inatakiwa awekwe
mwalimu aliyetulia na si hao wa kulipuliwa kwa kuwa, hawana muda wa
kumfundisha mtoto mpaka aelewe.Wakati
huo huo, Ofisa Elimu wa Sekondari katika halmashauri hiyo, Michael
Handu, alisema kuna haja kwa serikali kufanya marekebisho katika vyuo
vya ualimu kwa kuwa kuna tatizo. Aliongeza
walimu wanaopokewa wanakuwa hawana nia ya dhati ya ualimu, kwani baadhi
yao hawafanyi kazi ipasavyo wanaangalia masilahi zaidi.
Chanzo: Tanzania Daima
Ushauri: Serikali iwathamini walimu kwa kiasi kikubwa sana, ili na walimu wenye wito waweze kwenda kufundisha shule zenye uhitaji mkubwa wa walimu hasa vijijini na palipo na upungufu wa walimu! Lazima tufahamu kitu kimoja! Ualimu ni wito siyo lazima!!
0 comments:
Post a Comment
Asante kwa kusoma habari hii! Tafadhali acha tupia maoni yako HAPA!