Subscribe:

Ads 468x60px

Labels

“WASANII WA FILAMU TANZANIA MNATIA AIBU”-MZEE SMALL


MZEE Small amewarushia makombora wasanii wa filamu za Tanzania akisema kuwa wanatia aibu na asailimia kubwa hawajui wanachokifanya kwenye sanaa hiyo.

Mchekeshaji huyo mkongwe amesema kuwa kazi za wasanii hao nyingi hazina maadili na hazifai kuangaliwa na familia haswa yenye maadili ya kiafrika.

"Wasanii wa filamu wanajitahidi kuigiza kwani ukingalia walipoanzia na hapa walipofikia wamepiga hatua ingawa si kwa kiasi kikubwa kama wanavyojidai,"anasema msanii huyo.

"Tatizo lao kubwa ni maadili, hakuna maadili katika filamu zao ni aibu, kuna filamu mzazi huwezi kukaa na watoto wako kuangalia, wanaigiza mambo ya ajabu, nguzo walizovaa si za heshima, hili jambo waliangalie sana wanapotosha maadili ya mtanzania.

Nchi hii watu wanaishi kwa maadili na lazima yafuatwe sio watu wanakimbilia mambo ya nje ya nchi waliangalie upya suala hilo huku wakijiuliza hii nchi ina maadili?,anasema msanii huyo shabiki wa Yanga ya Dar es Salaam.

Amewaponda pia wasanii hao kwa kujiona mastaa kupita kiasi hali inayowafanya wavimbe vichwa na kupuuza hata ushauri wa waliowatangulia jambo ambalo amesema si zuri na haliwezi kuwajenga.

"Sioni kama wanapiga hatua na hiyo inatokana na kutokubali ushauri wa watu kama sisi, wao wanajiona wanafanya vizuri tu kumbe ndio wanazidi kuporomoka kisanii, mtu unayependa maendeleo lazima ukubali changamoto si kusifiwa tu kila siku."

Akizungumzia mustakabali wake Mzee Small anasema; " Kwenye Televisheni nimepumzika kwanza nafanya sana filamu, nimewaachia vijana ambao wanatamba hivi sasa ingawa najua hata nikiomba kazi ya kuigiza sasa hivi kwenye kituo chochote sipati kwa sababu vijana wengi wamekamata nafasi hizo hivi sasa."

Kuhusu ubora wa filamu nchini Mzee Small anasema baadhi zina ubora ingawa nyingi hazikidhi haja na maudhui yake yanafanana. " Unajua tatizo kubwa ni kwamba mtu anatoa filamu tatu au nne kwa mwezi, haiwezi kuwa bora kwa sababu ni lazima maudhui ya filamu zile yafanane kwavile upeo wa mtunzi wa filamu hizo lazima uwe mdogo kwa sababu hakujipa muda wa kufikiria kitu kipya, akatoa mfululizo, hapo ndipo wanapoharibu."

"Lakini vile vile ukiangalia upande mwingine huwezi kuwalaumu sana kwani tatizo kubwa linalosababisha yote hayo ni pesa, mtu anaona ni bora atoe filamu mfululizo ili apate pesa kwani maisha ya wasanii wa Tanzania ni tofauti na wenzetu nje ya nchi.

Lakini licha ya kuangalia maslahi zaidi wanatakiwa pia kubadilika na kutoa filamu zenye kiwango ili hata wanunuzi wa filamu hizo waridhike, sio wanatoa ili mradi filamu,anasema Small amezaliwa mwaka 1955 huko Kilwa na ana watoto watano.

0 comments:

Post a Comment

Asante kwa kusoma habari hii! Tafadhali acha tupia maoni yako HAPA!